Jana rais Magufuli amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa , ambapo baadhi ya wakuu wa wilaya amewapandisha na kuwa wakuu wa mikoa . Mabadiliko ya wakuu wa mikoa hao nikama ifuatavyo:
Mkoa wa Manyara - Mkuu wa mkoa ni Alexander Pasto Mnyeti alikuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru.
Mkoa wa Geita - Mkiu wa mkoa ni Robert Gabriel Lughumbi alikuwa mkuu wa wilaya Korogwe.
Mkoa wa Rukwa - Mkuu wa mkoa ni Joachim Leonard Wagambo alikuwa mkuu wa Wilaya Nanyumbu.
Mkoa wa Mara - Mkuu wa mkoa ni Adam Kigoba Ally Malima aliwahi kuwa kwenye baraza la mawaziri awamu ya nne.
Mkoa wa Mtwara - Mkuu wa mkoa ni Gerasius Gasper Bakyanwa alikuwa mkuu wa wilaya Hai.
Mkoa wa Dodoma - mkuu wa mkoa ni Bi Christine Solomoni Mndene alikuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini.
Lakini pia Raisi magufuli amemtea aliyekuwa IGP Erneste Mangu kuwa Barozi wa Tanzania na Azizi Malima na kusema kuwa vituo vyao vya kazi vitakuja kutangazwa badae .