Kamati ya Bunge la
Seneti la masuala ya usalama nchini Marekani imechapisha ushahidi
utakaotolewa na mkurugenzi aliyetimuliwa kazi FBI ambaye amesema Rais
Trump alimtaka mkurugenzi huyo kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa
masuala ya usalama.
James Comey alitoa uchambuzi wa ushaidi wa
mazungumzo kati yake na rais Trump aliyofanya naye mara tano wakati
Trump alipokuwa akirudia kutaka amsikilize na kumheshimu wakati ambapo
Comey anasema alikuwa akifanya kazi zake bila kuegemea upande wowote.Wakili wa Trump amesema rais Trump anahisi kuna ukweli kwa uthibitisho kuwa yeye mwenyewe binafsi hakuwa akichunguzwa kwa timu yake ya kampeni zake kuhusishwa na Urusi.
Maafisa wawili wanaohusika na usalama,Mike Rogers na Dan Coats wamewaambia maseneta kuwa hawakuwahi kulazimishwa kufanya jambo lolote ambalo liko kinyume na sheria.
- Trump amuonya mkuu wa FBI aliyefutwa James Comey
- James Comey anadaiwa kukataa kumtii rais Trump
- Trump atetea hatua ya kumfuta Comey
Hii ni moja ya majopo pamoja na idara ya sheria, kuchunguza ripoti za mashirika ya ujasusi ya Marekani kuwa wadukuzi wa Urusi waliingilia kati uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba.
Pia kuna uchunguzi kuhusu ikiwa kundi la kampeni ya Trump lilishirikiana na wadukuzi wa Urusi madai ambayo Urusi inayakanusha.
Tags
Kimataifa