Marekani imesema kuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika jaribio lake
la kwanza la mtambo wa kutungua makombora ya nyuklia ya masafa marefu.
Mtambo huo wa ardhini umefungwa katika kambi ya kijeshi iliyopo
Califonia kwaajili ya kujihami na vitisho ambavyo vimekuwa vikitolewa na
maadui zake ikiwemo Korea Kaskazini.
Aidha, Pentagon imesema kuwa jaribio hilo limefanyika baada ya Korea
Kaskazini kufanya majaribio yake ya makombora tisa ya masafa marefu
mwaka huu hivyo kutishia usalama wa nchi hiyo.
“Mfumo huu ni mhimu sana kwa ulinzi wa taifa letu na jaribio hili ni
uthibitisho mkubwa kwamba tuna uwezo wa hali ya juu wa kujilinda na
kutetea usalama wa raia wetu,” amesema Mkurugenzi wa kitengo cha ulinzi
wa makombora, Admirali Jim Syring.
Tags
Kimataifa