BREAKING NEWS: Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuuwa watuhumiwa wanne (4) wa mauaji huko Kibiti

Mkuu wa Oparesheni maalumu ya jeshi la polisi, Naibu Kamishna, Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi Juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda, ambapo askari polisi wakiwa katika doria walikutana na kikundi cha watu sita, watu hao baada ya kuona gari la polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.

Sabas anadai katika mapambano hayo yaliyodumu kwa nusu saa, polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watuhumiwa nne ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu. 

"Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji":- alisema Naibu Kamishna, Liberatus Sabas 

Mbali na hilo Naibu Kamishna, Liberatus Sabas amewataka wahalifu wengine kuacha mara moja vitendo hivyo na kusema vyombo vya usalama vipo kazini kuhakikisha usalama wa eneo la Pwani unakuwepo siku zote. 

Mpaka sasa ni zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha kwa kuuwawa wakiwemo askari polisi pamoja na viongozi mbalimbali hususani viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post