Picha za uchi zampa jina Ben Pol baada ya kampuni moja kujitokeza kumdhamini apige nyingi zaidi


Ben Pol

Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol amefunguka kwa kusema kuwa baada ya kusambaza mtandaoni picha zinazomuonyesha akiwa nusu mtupu na mng’ao wa mafuta, sasa amepata dili ya kuwa balozi wa mafuta ya kujipaka na kwa sasa wapo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo.

Ben Pol amekimbia kipindi cha Kwetu Flavor ya Magic Fm kuwa baada ya picha kusambaa, kuna makampuni yamemfuata  na kutaka kufanya naye biashara ya matangazo.

“Hapa sasa hivi tunaongea kuhusu majukumu yangu kama balozi, nione nina show ngapi katika hiyo event na mambo ya maslai inakuaje, nione matangazo ya runinga na mabango na nijue amount ya kazi yote ilivyo ni kiasi gani ninaweza kunufaika.Tukifikia muhafaka watu wataniona kwenye mabango, nimekoleza mafuta nimeweka na logo za hiyo kampuni,” amesema Ben Pol

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post