Moja ya stori ambazo zinatrend kwenye mitandao ya kijamii ni kifo cha aliyekuwa mume wa zamani wa Zari na Mfanyabiashara maarufu Uganda Ivan Don ambapo Zari amekuwa akipost picha na kinachoendelea msibani kwenye ukurasa wake wa Instagram jamba linalokosolewa na baadhi.
Sasa pamoja na picha za Zari kuwa gumzo leo May 30, 2017 muigizaji Wastara Juma ameandika ujumbe kupitia account yake ya Instagram akiwajia juu watu wanaomtukana Zari kwenye mtandao baada ya kupost picha zake akiwa kwenye msiba.
>>>”Ukimuona nyani kazeeka na bado anaishi ujue kakwepa mishale mingi saana mtanisamehe kwa masamiati huu Lakini mim ni mama sijawahi kusahau uchungu wa mwana na wala sijamsahau aliyenifanya niitwe mama lakini usiniulize kwanin sipo na niliyezaa nae ni mambo binafsi sana sio lazima kila mtu ajue Lakini akifa nitaenda na ikibidi kulia nitalia sababu alikuwa na bado atakuwa baba wa watoto wangu…..
“Lakini why why why mtu atukanweee weee asemwee kipindi kibaya cha uchngu na mawazo kama hiki hivi jamani mnajua kufiwa kweli wenzangu mbona hili la zari kutukanwa limenishinda kabsa kuvumulia…
“Mtazameni huyo mtoto mdogo kwenye pic anamtazama babaake kwenye pic aliyoishika huku akitabasam utafikiri anasema baba upo umeenda kutembea siku moja utaludi tuu Pangine Ajui hta maana kufa ailewi aelewi maskini Acheni basi fikirieni machungu yenu mpate hata robo ya maumivu wanayopata viumbe hawa #kufaanapesaavifanani Pole wafiwa @zarithebosslady Mungu amlaze mahali pema ivan ameen“ – Wastara.