Natamani Kuolewa lakini Sijapata Chaguo Sahihi


Niko na rafiki yangu hapa ananiomba nimshauri afanyaje maana anatamani kuolewa na mtu watakaependana kwa dhati. Tatizo anaowapenda wanamtenda, asiowapenda wanamjali sana..
Kwa hivi sasa ana umri wa miaka 27, ana boyfriend anaetaka kumuoa lakini anaogopa kuingia katika ndoa ambayo hana mapenzi ya kweli kwa mumewe. Wasiwasi wake ni kuwa mwisho atajikuta anazeeka akiwa single kwa kusubiria mru atakaependana nae.
Anahitaji moyo wake uridhike, na mtu atakaemuoa aridhike nae. Haamini kuwa kuna akubali kuolewa na aliepo harafu atajifunza kumpenda ndani ya ndoa. Na wana miaka mitatu ktk uhusiano na huyo alie nae. Hafeel kuongozana nae na hata kumtambulisha kwa marafiki.Naomba mnisaidie mawazo hapa wadau jinsi ya kumshauri ktk hili.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post