John Mnyika, Zitto Kabwe Walilia na Ufisadi wa Mchanga wa Madini Lakini Walipuuzwa



Rais John Magufuli aliunda Tume ya uchunguzi kuhusu usafirishaji wa mchanga wenye madini na ripoti imewasilishwa leo 24/05/2017 Ikulu jijini Dar Es salaam

Lakini pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa jambo hilo la kizalendo, niseme kwamba amechelewa Sana.

Kambi ya Upinzani kupitia waziri kivuli wa nishati na Madini Kamanda John John Mnyika aliwasilisha hoja binafsi kuitaka Serikali ya Ccm akiwepo Rais Magufuli akiwa waziri kuwasilisha mikataba yote ya madini bungeni na wabunge kuipitia na kuichambua kwa kina na kuifanyia marekebisho ya haraka kwa maslahi ya nchi yetu.

Wabunge wa CCM kwa kauli moja walikataa hoja hiyo ya Upinzani mwaka 2012 na mwaka 2013 kwa maslahi ya CCM. Walikataa hoja ya kuitaka Serikali kuweka hadharani mikataba na hivyo waliilinda serikali yao ya CCM kwa hofu ya kuwajibishwa.

Zitto Kabwe aliwahi kuhoji kuhusu usafirishaji wa mchanga nje ya nchi na mrahaba hafifu miaka ya 2007 ,2008 na 2009.Zitto aliibua kashfa ya Ufisadi ya Buzwagi akishirikiana na aliyekua katibu mkuu wa CHADEMA na mbunge wa Karatu Dk Slaa kwa niaba ya Kambi ya Upinzani. Spika wa bunge na bunge lilimfukuza Zitto Kabwe Bungeni kwa hoja kwamba amepotosha Bunge na Taifa badala ya kufanya utafiti na uchunguzi wa kina.

Upinzani hufikiria na kuona miaka 50 mbele wakati CCM huona kesho. Haya ya Leo Upinzani uliyasema na kuyaibua kwa vielelezo lakini Upinzani ulitukanwa kwamba nyaraka hizo ni za kufungia maandazi.

Ccm, wabunge wa CCM na Serikali ya Ccm acheni kusimamia maslahi ya CCM. simamieni maslahi ya Taifa kwa kizazi cha Leo na kesho.

Daniel Ezekiel Daniel(DED)
danielezekiel2222@gmail.com
ILEJE

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post