Moja
kati wasanii wakubwa hapa Bongo ambao walikuwa ni wachafu wa account za
Instagram ni pamoja na Diamond Platnumz. Ni msanii mkubwa Afrika mwenye
idadi kubwa ya wafuasi kwenye mtandao wa Instagram lakini page yake
hiyo ilikosa hadhi yenye kuendana na jina lake na ikawa yenye hadhi ya
page za kina Carry Mastory ama local artists.
Iko
wazi Diamond ana utajiri mkubwa wa mashabiki na fan pages za kutosha
ambazo zinaweza fanya promotion ya hatari kwenye ishu zake,mbali na hapo
ana ukurasa official wa kupost kazi zake ambao pia unaweza post
challenges,kuna Tik Tok, lakini pia ana media ambazo zina uwezo mkubwa
wa kusogeza kazi zake, alikuwa hana haja ya kupost mauchafu ambayo
yanaharibu image ya acc yake kusudi tu ionekane ngoma inasumbua kitaa.
Kizuri
Diamond ameacha kupost challenges kwenye ukurasa wake karibia project
zake 3 za mwisho, lakini kibaya zaidi mashabiki zake wana yale mawazo ya
hizo projects kuwa hajazifanyia promotion sababu wamezoeshwa kuona
mauchafu hayo (video za challenges) kwenye ukurasa wake.
Si
tu kuwa ameacha bali amefuta challenges nyingi kwenye ukurasa huo.
Niliwahi andika hapa hapa kuwa anacho kifanya si cha hadhi yake na kwa
hiyo akili kazidiwa hadi na mshindani wake Alikiba ambaye account yake
ni safi muda mwingi, huku nikitoa mifano mingine ya mastaa kama
Wizkid,Davido na Burna Boy namna walivyoachia page zao za habari zifanye
kila kitu ila watumiaji wa bando bana wakacomment matusi.
Instagram
ni moja ya taswira kubwa za celebrities,mfano juzi kati Diamond
alipostiwa kwenye ukurasa wa WASHINGTON FC, mashabiki wa timu hiyo
walikuwa hawamjui na suluhisho lilikuwa ni kukimbilia kutazama acc yake
kuona ni nani hasa, wakiishia kushangazwa na uwingi wa followers
alionao, imagine huyo anayechungulia acc anakutana na challenges kama
mia ndio aje ajue huyu ni fulani keshajikatia tamaa hapo mwanzo tu,vipi
ikiwa anakutana na show kama mia hivi,ni credit kubwa sana.
In short wasanii wetu inabidi wajue social media zao ni kwaajili ya Local Market au soko la nje.