Ishara Za Kuonyesha Kuwa Mpenzi Wako Ana Mchepuko

 


Ushawahi kuwa na hisia kuwa mpenzi wako labda ana mchepuko? Umekuwa ukijaribu kufanya utafiti wako wa kina lakini kila ukijaribu kupekua unaambulia patupu?

Ok. Leo kwa haraka tumekuja na ishara ambazo unaweza kuziangalia kwa mpenzi wako kama anachepuka au la.


Hapa Nesi Mapenzi tuko hapa kukujuza. Hivyo basi jukumu lako pia uhakikishe unawajuza marafiki zako. Ukiwa unashuku rafiki yako anamegewa basi usisite kumrushia na yeye chapisho hili pia yeye afunguke macho.


Well, mpenzi wako akiwa anachepuka basi inamaanisha jambo moja, wewe utakuwa ni number 2 automatic. Hivyo usikubali kamwe kuwekwa katika hali kama hii. Zama nami!


#1 Huwa anasumbuliwa na wasiwasi.


Ukitaka kujua kama mpenzi wako anachepuka, basi mwambie akupeleke zile sehemu ambazo anakuwa akitembea wikendi ama nyakati za jioni. Hapa utamwona kwanza akianza kutoa visababu visivyo eleweka. Na pindi akikubali kutoka na wewe basi hatakuwa makini na wewe bali atakuwa na wasiwasi asije akapatikana ghafla na mchepuko wake.


#2 Sikiliza moyo wako.

Ok, hii ni ishara ambayo iko ndani ya fikra zako. Ijapokuwa watu hawaamini kuwa fikra zako zinaweza kukupatia jawabu, ukweli ni kwamba kuna asilimia 100 kuwa unaweza kuwa kweli. Mfano umekuwa na huyu mwanamke kwa kipindi cha mwaka mzima. Halafu ukaona matendo yake yamebadilika ghafla. Unamwona anafalia nguo za kurembesha, anapaka marashi akiwa anatoka out na kadhalika. Hapa fikra zako zikikuambia kuwa anakucheat basi kunaweza kuwa na ukweli ndani yake. [Soma: Hatua 10 za kufanya urudiane na ex wako]


#3 Hapatikani wikendi.

Kwa kawaida huwa tunafanya kazi kuanzia jumatatu hadi ijumaa. Hivyo basi wikendi tunakuwa tuko huru kupumzika. Lakini ukiona kuwa mpenzi wako ukijaribu kumwambia mkutane siku za wikendi lakini anakupa visababu kuwa ana shughuli za kufuatilia na hatapatikana basi ujue hapo kuna mchezo anaucheza.


#4 Anapost picha akiwa na wanaume wengine.

Hii pia ni ishara muhimu ya kuchunguza. Najua mwanaume alpha hana tabia za kuwa na wivu. Lakini ukiona kuwa mara kwa mara anaweka picha za huyu mwanaume halafu ukimuuliza anakwambia kuwa ni cousin yake basi anza utafiti wako.


#5 Hasisimkwi na wewe.

Mwanamke ameumbwa kuwa na hisia. Hivyo kikawaida ukiwa na mwanamke kuna hisia tofauti tofauti ambazo atakuwa anakuonyesha. Hii ni kuanzia kulia, kucheka, kukasirika, kunungunika na kadhalika. Lakini ukiona kuwa hakuna hata hisia moja unaweza kuzua kutoka kwa huyu mwanamke basi fahamu anakuendea kinyume. Mara nyingi hii ni ishara kukuonyesha kuwa hauna manufaa yeyote kwake na anajua kuwa kuna mwingine ambaye anaweza kumsisimua wakati wowote. [Soma: Maswali 40 ya kumuuliza mwanamke katika deti]


#6 Hashughuliki kukupatia changamoto.

Wanawake ambao wanawapenda wapenzi wao huwa wanapenda kuwapa changamoto maishani. Kwa mfano ukifungua biashara mpya mwanamke atakupa changamoto kwa kukuuliza maswali ambayo hata hukuwa umeyafikiria. Lakini ukiona mwanamke hana time na kutaka kujua maendeleo yako kimaisha ama kiuchumi na wala hajawahi kukuuliza chochote basi jua kuwa unamegewa.


#7 Simu yake ni siri yake.

Mwanamke ambaye anakucheat mara nyingi anakuwa ameweka password kila mahali. Kuanzia whatsapp, facebook hadi messenger. Na ukimwambia akufungulie utumie calculator basi atakuwa akikuuliza kila dakika unafanya nini.


#8 Marafiki zake wanakuwa na tabia tofauti wakiwa na wewe.

Hapa mara nyingi ni kuwa marafiki zake washajua kuwa wewe unamegewa. Lakini wanashindwa kukuweka kando na kukuambia kwa kuwa wameweka ni siri kati yao na mpenzi wao. [Soma: Sms ambayo itamfanya mwanamke akutamani]


Ok. Hizi ni baadhi ya ishara kuonyesha kuwa mpenzi wako ana mchipuko. Kabla ya kuchukua hatua yeyote hakikisha kwanza una uhakika dhabiti kuwa mpenzi wako anakucheat. Usikimbilie kuachana naye kama anakataa kukufungulia simu. Utafiti kwanza ndio muhimu.


Mafanikio kwako.


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post