Maelfu ya mashabiki ya Barcelona waliacha vitanda vyao usiku wajana kuamkia leo Jumatano na kuingia barabarani kuandamana wakielekea Nou Camp wakionyesha msisitizo wao wa kutofurahishwa na namna bodi ya klabu hiyo inavyoshukhulikia sakata la legend wao Lionel Messi.
Nyota huyo wa Argentina amefikisha maombi yake kwa uongozi wa Barcelona kutaka kuondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu na mafanikio makubwa.
Nyota huyo wa Argentina amefikisha maombi yake kwa uongozi wa Barcelona kutaka kuondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu na mafanikio makubwa.
Inadaiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 tayari ameshafanya mazungumzo na kocha mpya wa Barcelona, Ronald Koeman juu ya adhima yake ya kuondoka.
Wakati sakata la Messi likizidi kushika vichwa vya habari ghafla kuna taarifa zimevuja kupitia Radio yakisikika mazungo kocha Ronald Koeman dhidi ya Luis Suarez juu ya hatma yake katika kikosi cha Barcelona hali iliyozidi kuzua taharuki.
Suarez ambaye ni rafiki wa karibu na Messi, ni miongoni mwa wachezaji wanne ambao wameambiwa na kocha, Koeman kupitia mawasiliano ya simu kuwa hawahitaji ndani ya klabu.
Inadaiwa huwenda maamuzi ya kocha huyo wa zamani wa Everton kuwaambia Suarez na wenzake kuwa hawahitaji kikosini na watafute mlango wa kutokea inaweza kuwa sababu iliyochangia maamuzi ya Messi kuomba kundoka Barcelona.
Tags
SOKA ULAYA