Kamati imeeleza kuwa kulikuwa na mapungufu kwenye mkataba wa mchezaji huyo ambapo kuna ukurasa wa saini umekutwa umekatwa na tarehe zikiwa zimepishana.
Pia amesema kuwa tofauti kwenye tarehe ndani ya mkataba huo ni kwamba ipo moja inaonyesha kuwa alisaini tarehe 20 mwezi wa tatu na nyingine inaonyesha tarehe tofauti jambo ambalo limempa ushindi Morrison.
Ameongeza kuwa ilichukua muda mrefu kwa kuwa kesi ilikuwa inahitaji umakini huku akizitaka timu kuwa makini kwenye masuala ya mikataba kwa kuwa wamepoteza muda mrefu kwa jambo ambalo halikuwa na ulazima kutokea iwapo kungekuwa na umakini.
"Tumepoteza muda mwingi kwa ajili ya suala hili, ninadhani ingekuwa maamuzi yangu binafsi ningechukua uamuzi tofauti kabisa katika suala hili ila kwa kuwa kazi yetu tumemaliza basi mchezaji atakuwa huru kuchagua wapi anakwenda.
"Kuhusu kesi yake na mkataba wake wa pili hilo halikuwa chini yetu sisi tulikuwa tunakiliza shauri la mkataba wa kwanza jambo la yeye kusaini sehemu nyingine hilo ni kosa mchezaji mwenyewe amekiri.
"Kwa kufanya hivyo anapelekwa Kamati ya Maadili na haina uhusiano na kesi ambayo tulikuwa tunaisikiliza sisi, yeye ni mchezaji huru kwa kuwa ameshinda," amesema.
Tags
Michezo