Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia HESLB kuwa mfumo wa uombaji wa mkopo kwa njia ya mtandao utakuwa wazi kwa siku 40 kuanzia Jumanne, Julai 21, 2020 hadi Jumatatu, Agosti 31, 2020.
Tunawashauri wanafunzi wahitaji kutumia muda wa sasa hadi mfumo utakapofunguliwa (Julai 16, 2020 hadi Julai 21, 2020) kusoma ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Mwaka 2020/2021’ unaopatikana kuanzia sasa katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) katika lugha za Kiswahili na Kiingereza.
Mwongozo huu unatoa maelekezo ya kina kuhusu sifa, utaratibu na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa upangaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.
Aidha, baada ya kuusoma, tunasihi waombaji mikopo kuhakikisha wanaandaa nyaraka zote muhimu kama zinavyoelekezwa katika Mwongozo huo.
Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM
Alhamisi, Julai 16, 2020
poa sana
ReplyDelete