SEHEMU Tano za Mwili Wako Ambazo Hupaswi Kuzigusa kwa Mkono..!!!


Mikono yetu ni kiungo muhimu sana kinachoweza kupapasa karibu asilimia 99 ya miili yetu bila shida, lakini tafiti zimeonesha kuwa ni hatari zaidi kwa afya yetu kushika sehemu kadhaa hususan sehemu hizi tano.

Katika hali ya kushangaza, utafiti uliofanywa na jopo lililoongozwa na Profesa Kelly Reynolds wa Chuo cha Zuckerman College of Public Health kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha Arizona, unataja maeneo hayo ya mwili. Baadhi ya maeneo hayo ni haya yafuatayo:

Macho

Kama jicho lako halikulazimishi kulishika labda pale unatoa uchafu wa aina yoyote kwa namna inayofaa, hakikisha hauligusi kabisa. Hii ni kwa sababu mikono yetu inabeba mambo bakteria ambao wanaweza kudhuru macho yetu taratibu na kudhurika bila kufahamu haraka.

Uso

Uso ni sehemu ambayo ni rahisi sana kupeleka mkono mara kwa mara. Ni ngumu sana kuacha kufanya hivyo hususan kwa tunaofanya kazi za kutoa jasho au kutembea sehemu ambazo zinatoa jasho. Pamoja na mambo hayo, wataalam wamebaini kuwa ngozi ya uso ni ngozi ya kipekee na inapaswa kutunzwa kwa uangalifu zaidi. Mikono yetu ambayo hubeba mafuta mafuta pamoja na bakteria inaweza kudhuru ngozi zetu za uso.

Mdomoni (Nje na Ndani)

Utafiti zilizofanywa hivi karibuni nchini Uingereza umebaini kuwa mtu ambaye ameboreka (bored) kazini hushika maeneo ya mdomoni zaidi ya mara 23.6 kwa saa moj. Hali hii ni tatizo kubwa kwani utafiti umebaini kuwa robo tatu ya bakteria wabaya hupitia kwenye mdomo.

Ndani ya Pua

Kuna watu ambao kuchokonoa mapua yao ni sehemu ya tabia iliyojengeka. Kwa bahati mbaya, tafiti za kitabibu zimebaini kuwa watu wanaochokonoa pua zao kwa vidole wako katika hatari kubwa zaidi ya kushambuliwa na bakteria (staph bacteria) zaidi ya wale ambao hawafanyi hivyo.

Ngozi ya chini ya kucha

Ni kosa kubwa kutunza kucha zako kuwa ndefu kiafya. Kucha hubeba uchafu hata ule ambao huwezi kuuona kwa macho, bakteria wanaweza kujificha chini ya ngozi za kucha yako. Bakteria hao wanaweza kuwa chanzo kikubwa cha kuharibu afya yako. Hivyo, jitahidi kutofuga kucha, hakikisha kucha zako ni fupi kwa kiasi cha kutosha ili usiipe nafasi bakteria kuishi.

Lakini kama unafuga kama urembo, unapaswa kuwa na matunzo ya ziada ya namna ya kupambana na bakteria ambao huwaoni kwa macho.


Note: Sehemu za siri ni shemu ambazo kila unapotaka kuzigusa fahamu kuwa ni sehemu ambazo zikiguswa na bakteria uliowasomba na mikono yako zinaweza kukusababishia madhara makubwa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post