Nandy, Tanasha Watangaza Hali Ya Hatari

Mastaa wa kike wa muziki Afrika Mashariki, Faustina Charles ‘Nandy’ na Tanasha Oketch Donna, wametangaza hali ya hatari.

 

Tanasha ambaye ni mrembo kutoka Nairobi, Kenya na mzazi mwenza wa mwanamuziki Nasibu Abdul, ‘Mondi’ ndiye ametangaza kwamba yeye na Nandy wana jambo lao kubwa linakuja.Tanasha aliposti video kwenye ukurasa wake wa Insta akitaka mpambano wa kikazi kati yake na Nandy.

 

“Hellow natumaini mko salama, kwa kuzungumzia Afrika Mashariki, tunataka kuonesha ni vitu gani wasanii wa kike tunavyo.



“Hivyo tunakwenda kufanya mpambano wa kikazi na Nandy kutoka Tanzania au unaonaje Nandy?’’ Alisema Tanasha kwenye video.Baada ya kuposti video hiyo, Nandy aliibuka na kumjibu Tanasha kuonesha amekubali.“Ohh yeah,’’ alijibu Nandy na kumtagi Tanasha.

 

Tanasha na Nandy wamekuwa na ukaribu mno kwenye Mtandao wa Instagram, kwani wamekuwa wakichati kinoma.Habari ni kwamba, kuna ngoma ambayo wamefanya kwa pamoja na itatoka mwaka huu.

Hii si mara ya kwanza kwa wanamuziki kufanya mpambano, kwani hata nchi za nje, wanamuziki wengi wamekuwa wakifanya mpambano kwa lengo la kuendelea kukuza kazi zao na zionekane.

 

Nandy na Tanasha ni wanamuziki ambao wana vipaji vikubwa, wote wanajua kuimba na kila mmoja ametoa kazi kali.Kwa sasa Tanasha anakimbiza na ngoma yake ya Sawa na kwa upande wa Nandy anafanya vizuri na ngoma ya Acha Lizame akiwa amemshirikisha C.E.O wa Lebo ya Konde Gang Worldwide Music, Rajab Abdul ‘Harmonize’

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post