DAR: Baada ya kudaiwa kuwa wazazi wa mchumba wake Faustina Charles ‘Nandy’ hawamtaki, msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, William Lyimo ‘Billnass’ ameibuka na kueleza ukweli wa mambo.
Mara baada ya Nandy kuchumbiwa ghafla na tukio kurushwa na Televisheni ya E, maneno yaliibuka mengi ambapo wengine walienda mbali zaidi kwa kusema kwamba, msanii huyo alifanya hivyo bila kuwa na ndugu wengi kwa sababu hakubariki ukweni.
“Hakubaliki. Ndio maana umeona Billnass kaona afanye tu kwenye kipindi cha televisheni na hakuna ndugu waliohudhuria tukio hilo. Nasikia hawataki ata kumuona Billnass,” yalikuwa ni madai ya wambea wengi kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Baada ya kuona maneno yamekuwa mengi, RISASI lilimtafuta bwana harusi mtarajiwa ambapo baada ya kupatikana, alisema haoni tatizo yeye kumfanyia surprise mpenzi wake kwa sababu hicho ndicho kitu anachokipenda.
“Unajua ukikaa na kuanza kusikiliza maneno ya mtandaoni, utaumiza akili yako bure, kwa sababu asilimia kubwa ya watu wanaoongea hivyo, hawajitambui vizuri.
“Sioni ajabu mimi kumfanyia surprise mpenzi wangu, kwa sababu najua nini anapenda, pia tunafahamu kabisa sasa hivi kuna Corona, hivyo ingekuwa ngumu mimi kualika ndugu na wazazi usiku ule kwa sababu tungekiuka sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali kuhusu huu ugonjwa wa Corona,” alisema Billnass na kuongeza:
“Kuhusu kukataliwa ukweni, sidhani kama ni kweli, lakini pia wakwe zangu mimi ni watu wa dini sana, hivyo nisingependa kuwaongelea sana kwenye media yoyote ile kwa sababu ninachokijua mimi ni kwamba, wananipenda kama mtoto wao na wamenikubali.”
Billnass na Nandy wametoka mbali, waliwahi kuwa wapenzi wakaachana na sasa wamerudiana kwa kasi na jamaa kaona amvishe pete kabisa.
Endapo mipango yao itatimia, kapo hiyo itakuwa baab’kubwa kwani wote wawili ni wasanii wa Bongo Fleva