Msanii nguli wa Bongo Fleva, Madee 'Seneda' ameshindwa kuficha hisia zake baada ya kuona picha ya msanii mwenzake wa kitambo, Chid Benz katika mitandao ya kijamii ikimuonesha ameongezeka tofauti na awali.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Madee ameandika kuwa picha hiyo ndiyo namna anayostahili kuwa nayo Chid Benz kwani mwili huo ndio alikuwa anaufahamu kutoka kwake.
"Hii ni picha mpya nimeikuta uko mitandaoni. Nafikiri Mungu amezisikia dua zetu, huu ndio mwili ninaoujua mimi toka kwa Chid Benz!!. Mungu azidi kukuongoza bro!!", ameandika Madee.
Katika picha yake hiyo kwenye mtandao wa Instagram, Chid Benz ameandika, "kila siku ni siku nasisitiza. Unaweza kuwa vyovyote ukiweza, na ukafanya yote unayoweza. Badilika ili ubadilishe unachowaonesha".
Chid Benz amekuwa na safari ndefu katika muziki wake kwenye miaka ya hivi karibuni, kutokana na mara kadhaa kuonekana akijiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya. Lakini hivi sasa ameonekana kutoka kabisa kwenye janga hilo, jambo ambalo wengi miongoni mwa wasanii wenzake na mashabiki wake walikuwa wakitamani kuona
Tags
WASANII