Jack Wolper ''Natamani Kuacha inaniharibia Sana''

Msanii wa filamu na mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper, amesema yeye ni miongoni mwa watu wanaopitia changamoto kubwa hususani kwenye mahusiano yake pale anapotoa support kwa wasanii.

Wolper amefunguka hilo kupitia Friday Night Live jana Aprili 24, 2020, ambapo amekiri kuwa kila akipost kukubali kazi za wasanii huwa inampa shida kwenye mahusiano yake kutokana na mtazamo uliopo kwa wasanii.

''Unajua inaniharibia sana mpaka natamani kuacha ila nimezoea inabidi tu niendelee na pia mashabiki wanavyotukana ukifanya jambo inaonekana kama kweli sasa kiasi kwamba mtu unayekuwa naye anakosa imani'' - Wolper.

Miongoni mwa wasanii aliopost kazi zao na kupata mitazamo tofauti ni Marioo, Harmonize, Ibraah na wengine lakini analazimika kufanya hivyo kwasababu nyimbo zao unakuta zimemgusa yeye au zinakuwa na ujumbe wa kuelimisha zaidi.

Wolper amesema kwasasa filamu hazilipi kama ambavyo kazi yake ya ubunifu wa mavazi inavyompaka pesa lakini pia ameona soko kwenye series hivyo anaweza kufanya chochote.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post