Diamond Platnumz amesimulia upande wake wa kilichofanyika kati yake na Tanasha Donna .msanii huyo aliyafichua yote yaliofanyika katika mahojiano na Wsafi TV ambapo amesema palitokea kutoelewana kati yake na Tanasha kabla ya wawili hao kuamua kuachana .
“ kwa kweli mimi na Tanasha hatuko pamoja . kulikuwa na mambo ambayo yalituzidi kiuwezo na tukaamua kama watu wazima na wastaarabu kuachia kila mmoja space yqake . na sio kuhusu kufumaniana ..hilo halikuwahi kufanyika’
Aliongeza kwamba wakati wa uhusiano wake na Tanasha kila jambo lilikuwa shwari .
‘Uhusiano wangu naye ulikuwa mzuri sana na nilikuwa nimetulia kwa sababu mambo ya ujana wangu niliyaweka kando .Tulikaa pamoja kama familia na kujadili kuhusu mustakabali wetu lakini hatukuafikiana kwani kila mtu alitaka alichotaka . iwapo mola amepanga basi huenda tukarudiana’
Aliongeza kwamba alikuwa na mpango wa kufunga ndoa na Tanasha na wala mpango huo sio utani wala maigizo kwa upande wake .
“ Nilitaka kumuoa Tanasha ,asilimia 100 .lakini labda haikuwa katika mpango wa Mungu ,kuna vitu ambavyo hatukuafikiana kuvihusu’.
Msanii huyo pia alithibitisha kwamba Tanasha alikuwa amesilimu na kujiunga na dini ya kiislamu
“ Tulikuwa Kigoma na akasilimu nikamuambia Ricardo Momo ( maneja katika WCB) kwamba akimshawishi afanye hivyo basi nitamlipa . Hakumlazimisha lakini alimfunza na baadaye aliponiambia kwamba anataka kusilimu nilimtaka afikirie kwanza kisha aje aniambie na akanieleza kwamba alikuwa na uhakika .
Katika mahojiano na True Love wiki chache zilizopita Tanasha alisema alimuacha Diamopnd kwa sababu ya tabia yake ya kuwa an wapezi wa pembeni na familia yake kila mara ilikuwa ikiingilia uhusiano wao .
Wawili hao walikuwa wametangaza kwamba wanegufunga ndoa Fneruari tarehe 14 mwaka wa 2019 tarehe kama hiyo ambapo Zari alitengana na Diamond mwaka wa 2018 .Baadaye waliahirisha tarehe hiyo hadi mwaka huu lakini harusi yao haikufanyika
Tags
WASANII