Bill Nas awatamani Cassper, Drake

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, William Lymo ‘Billnass’ amesema anatamani kufanya kolabo na wasanii kama Cassper Nyovest na Drake.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Billnass amesema kuwa, amekuwa akitamani kufanya kazi na Cassper Nyovest kutoka Afrika ya Kusini na Drake kutoka Marekani ambao wote ni marapa walio na heshima kubwa.

“Mimi naimba na kuchana na nimekuwa nikiwatazama sana wasanii kama Cassper na Drake, kwani wanaujua muziki wa kuchana na wanafanya vizuri sana, natamani siku moja nifanye nao kazi,” alisema Billnass.

STORI: Happyness Masunga

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post