Baraza la sanaa la Taifa "BASATA" wamesema wanalifuatilia suala la msanii Abdu Kiba kuvuja kwa video isiyokuwa na maadili katika mitandao ya kijamii.
Katibu Mkuu wa Basata Geofrey Mngereza amesema kwa sasa yupo kwenye kikao na COSOTA lakini anawaagiza watu wake kufuatilia suala hilo.
"Leo siku nzima nipo kwenye kikao na Cosota na video yake bado sijaiona lakini nawapa watu wangu waanze kuifuatilia, siwezi kudhibitisha au kuhakikisha kama ni yeye au sio yeye, lazima mtu uanze kufuatilia kwanza kisha tutoe majibu" amesema Geofrey Mngereza
Tags
Udaku