NYUMBA ZA WALIMU ZAGEUKA MANDANGURO HUKO SHINYANGA


Diwani wa Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga, Hassan Mwendapole amesema majengo ya nyumba za Walimu katika Shule ya Mwasele hivi sasa yamekuwa kama danguro, hali ambayo imepelekea Wanafunzi kupata ujauzito na kushindwa kuendelea na masomo

Mwendapole amesema, “Nyumba hizi za Walimu katika Shule ya Sekondari Mwasele zilijengwa tangu mwaka 2011 na sasa kuna mapagale tu, na yameshageuka kuwa kama guest house. Zinatumika kwa ngono na kusababisha kuwapo mimba za wanafunzi"

Inadaiwa kuwa, ujenzi wa majengo hayo ya nyumba mbili za Walimu bado haujakamilika, lakini yamekuwa yakitumika kufanya vitendo hivyo na baadhi ya Wanafunzi wamekamatwa wakifanya ngono

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post