SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wamekuwa wakishinda dakika za usiku kutokana na wachezaji wake kutokuwa makini ndani ya uwanja.
Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wapo nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 19 na kujikusanyia pointi 50 kibindoni.
Kwenye mechi mbele ya Namungo FC ya Lindi ambapo Simba ilishinda mabao 3-2 Meddie Kagere alifunga bao la ushindi dakika za lala salama pamoja na ule dhidi ya Polisi Tanzania ambapo Ibrahim Ajibu alifunga bao la ushindi dakika za lala salama na Simba ilishinda mabao 2-1 zote Uwanja wa Taifa.
Sven amesema:"Tumekuwa tukishindwa kumaliza mchezo mapema kutokana na wachezaji wangu kushindwa kuongeza umakini zaidi wa kutumia nafasi ambazo wanazipata, nimeligundua hilo na ninalifanyia kazi kwa ukaribu,".

Tags
Michezo