Niyonzima amewasili leo mchana akitokea kwao Rwanda alipokuwa akiitumikia AS Kigali baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Yanga.
Kiungo huyo amepokelewa na Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli aliyeambatana na Afisa Mhamasishaji wa timu hiyo Antonio Nugaz.
Mara baada ya kuwasili Niyonzima amesema kurejea kwake nchini ni maalum kwa ajili ya Yanga.
Niyonzima amesema anashukuru Mungu aliondoka Yanga akiwa salama na anarejea akiwa salama kuzidi kuipa nguvu timu yao.
Kiungo huyo amesema hana wasiwasi katika kurejea kwake Yanga kutokana na anaungana na kocha Charles Mkwasa na wachezaji wenzake baadhi ambao anajuana nao.
Akizungumzia mechi ya Januari 4 dhidi ya Simba amesema hiyo ni mechi kubwa ambayo anaiheshimu na wala hana wasiwasi na mchezo huo.
Kiungo huyo mara moja amewahishwa kambini kwenda kuungana na wenzake tayari kwa mazoezi ya leo jioni.
Niyonzima anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Yanga katika dirisha dogo akitanguliwa na washambuliaji wazawa Ditram Nchimbi, Tariq Seif, beki Adeyun Saleh pamoja na mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Yipke Garmien
Tags
Michezo