Mo Dewji akutana na Rais wa FIFA na kufanya naye mazungumzo


Wakati Simba ikitarajiwa kushuka dimba la Taifa leo saa moja usiku kuikaribisha Namungo FC kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, Mohamed 'Mo' Dewji, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), Gianni Infantino, katika makao

Katika mazungumzo yao, wawili hao waligusia mipango ya Fifa kuendeleza soka barani Afrika, Dewji akieleza matumaini yake juu ya maendeleo ya mpira wa miguu barani katika uongozi wa Infantino.

"Kwa kweli, nimefurahishwa sana kwa dira na shauku ya kuendeleza mpira wa ushindani na shauku Afrika. Nia ya Fifa ni kuboresha maendeleo ya mpira.

"Najua chini ya uongozi wa Gianni, mpira wa miguu kwenye bara letu, utaenda 'next level' (utapiga hatua zaidi)," Dewji alieleza baada ya mazungumzo yake na bosi huyo wa Fifa.

Aidha, Dewji alimkabidhi Infantino jezi ya Simba ikiwa imeandikwa jina la rais huyo ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupiga vita rushwa michezoni na ufujaji wa fedha uliokuwa ukifanywa ndani na nje ya shirikisho hilo kwa wanachama wake.

Dewji, mmoja wa mabilionea vijana barani Afrika, ameifanya Simba kuwa miongoni mwa klabu zinazoendeshwa kwa kisasa Afrika na sasa inatajwa kama timu inayotarajiwa kuwa tishio ndani ya miaka michache ijayo barani Afrika.

Katika hatua nyingine Balozi wa Simba jijini London, Salim Kikeke jana alikutana na Mkurugenzi wa Mpira wa Miguu wa QPR, Les Ferdinand na Mkurugenzi wa Ufundi ambaye amewahi kuwa kocha wa timu hiyo, Chris Ramsey kujadili namna klabu hiyo itashirikiana na Simba katika maendeleo ya soka la vijana.

Hatua ambayo Klabu ya Simba imeelezea kuwa "mambo makubwa yanakuja hivi karibuni."

Simba ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 41, baada ya kushuka dimbani mara 16 msimu huu, leo itaanza raundi ya pili ya ligi hiyo kwa kuikaribisha Namungo FC ya mkoani Lindi.

Simba itashuka dimbani ikitoka kuichapa Mwadui FC mabao 2-1 kwenye mechi ya Kombe la FA, wakati Namungo iliyopo nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya kucheza mechi 15 za raundi ya kwanza, nayo ikipata ushindi kama huo dhidi ya Biashara United katika michuano hiyo ambayo bingwa huiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Hata hivyo, kuelekea mechi hiyo wakati uongozi wa Namungo ukieleza wanatambua Simba ni timu kubwa na wanaiheshimu, Kocha Mkuu wa 'Wekundu wa Msimbazi' hao, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amesema tayari ameshabaini licha ya kwamba wapo kileleni mwa msimamo wa ligi, lakini hakuna timu ndogo na amebaini ugumu anapokutana na timu hizo.

Sven ambaye ameiongoza Simba kwenye mechi sita za ligi dhidi ya Lipuli FC, KMC, Ndanda, Yanga, Mbao na Alliance FC na kudondosha alama mbili tu kati ya 18 alizopaswa kuzivuna, amesema ugumu wa ratiba pamoja na changamoto kali wanayokutana nayo wanapocheza na wapinzani wao, umempa mbinu mpya ya kuweza kuzikabili.

“Wakati nakuja hapa nchini nilifikiri kila kitu kitakuwa rahisi tu, lakini nimegundua ni tofauti kabisa, ligi hii ni ngumu na timu zote zinapambana," alisema.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post