MSHAMBULIAJI chipukizi wa Tanzania, Kelvin John ‘Mbappe’, anajiunga
rasmi na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambayo nahodha wa timu ya taifa
ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta, alikuwa akiichezea kabla ya kujiunga
na Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.
Kelvin ambaye pia anaichezea timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Ngorongoro Heroes ya Tanzania, amekamilisha dili hilo la kujiunga na Genk.
Meneja wa mchezaji huyo Mbaki Mutahaba amesema, uongozi wa Genk umevutiwa na uwezo wa kijana huyo na kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa sasa ni umri tu.
Mchezaji huyo atafikisha miaka 18 baadaye mwaka huu na kwa sasa anaendelea na masomo katika chuo cha Brooke House nchini Uingereza.

Tags
MICHEZO KIMATAIFA