Ratiba ya 16 Bora Klabu Bingwa Ulaya, UEFA

Manchester City wataminyana na Real Madrid wakati mabingwa watetezi Liverpool watachuana na Atletico Madrid katika hatua ya 16 ya Klabu Bingwa Ulaya maarufu Champions League .

Chelsea wao watavaana na Bayern Munich huku Tottenham wakipangiwa RB Leipzig.

Borussia Dortmund watapambana na Paris St-Germain wakati Napoli take on Barcelona.

Mechi za raundi ya kwanza zitapigwa Februari 18, 19, 25 na 26, huku mechi za raundi ya pili zikitarajiwa kuchezwa Machi 10, 11, 17 na 18.

Fainali ya msimu huu itapigwa Mei 30 katika uwanja wa Ataturk Stadium jijini Istanbul,Uturuki uwanja ambao Liverpool walinyanyua kombe hilo kimaajabu mwaka 2005 baada ya kuifunga AC Milan.

Droo ya 16 bora

Borussia Dortmund v Paris St-Germain

Real Madrid v Manchester City

Atalanta v Valencia

Atletico Madrid v Liverpool

Chelsea v Bayern Munich

Lyon v Juventus

Tottenham v RB Leipzig

Napoli v Barcelona

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post