Mwanamke Amuua Mpenzi wake Baada ya Kumfuma Akimeza ARVs


Mwanamke mmoja katika Wilaya ya Hoima, Uganda anashikiliwa na Polisi akidaiwa kumuua mpenzi wake Emmanuel Tumusiime kwa kumpiga na shoka kichwani baada ya kumfuma akimeza dawa za kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi (ARVs).

Msemaji wa Polisi Hoima Julius Hakiza amesema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa Emmanuel mwenye umri wa miaka 35 alishambuliwa mpaka kuuawa nyumbani kwake katika Mji wa Kigorobya majira ya saa kumi na mbili jioni.

Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Monitor la Uganda, mwananmke huyo alipogundua kwamba Mpenzi wake amefariki alifunga nyumba na kupanda Bodaboda mpaka kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Hoima na kuripoti kuwa amemuua Mpenzi wake.

Hakiza ametoa wito kwa Watu wenye Virusi Vya UKIMWI kuwapa taarifa Wapenzi wao ili wawe wanahudhuria pamoja Hospitali na kupewa ushauri nasaha kwani kuwa na UKIMWI sio mwisho wa Maisha.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post