KOCHA MPYA WA ARSENAL AANZA NA MIKWARA


MIKEL Arteta ametangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Arsenal akitwaa mikoba ya Unai Emery aliyefukuzwa ndani ya klabu hiyo baada ya kudumu kwa miezi 18 kutokana na kuwa na mwenendo mbovu ndani ya timu.
Arteta alikuwa mchezaji wa zamani wa Arsenal na kabla ya kujiunga klbuni hapo alikuwa akifanya kazi na Pep Guardiola ndani ya Manchester City.
Kandarasi yake ndani ya Arsenal ni ya muda wa miaka mitatu na nusu na imethibitishwa na uongozi wa timu hiyo ambayo ilikuwa inasimamiwa na Kaimu Kocha Mkuu wa muda, Freddie Ljungberg.
Arteta amesema kuwa ni furaha kwake kuwa ndani ya Arsenal kwani ni timu kubwa na yenye heshima.
"Kwangu ni furaha na heshima kuwa ndani ya timu kubwa. Nina amini nahitaji kufanya mambo makubwa nami nina amini tutaleta ushindani na kuleta mataji ya kutosha na tutajadili na viongozi kuona namna ya kuwa bora." amesema

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post