FIFA KUJENGA UWANJA MMOJA TANZANIA


WALLACE Karia, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amesema kuwa FIFA wameahidi kujenga Uwanja mmoja hapa nchini.

Karia ameyasema hayo leo kwenye mkutano mkuu wa TFF unaofanyika ukumbi wa BOT ambao umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa mpira.

"FIFA wameahidi kujenga uwanja mmoja hapa nchini na tumekubaliana kujenga vituo viwili vya Soka (Technical Centres) kwa maeneo ya Tanga na Kigamboni-Dar es Salaam, ujenzi ambao mchakato wake umeshaanza na mapema mwakani ujenzi utaanza," amesema

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post