Kaimu kocha mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa amelazimika kutolea ufafanuzi wa kiwango cha timu yake kilichooneshwa katika mchezo dhidi ya Biashara United Desemba 30 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“Kabla ya kucheza tumekuwa na safari ndefu kama mnakumbuka kabla hatujacheza mechi yetu Mbeya tulikuwa na wastani wa safari ya saa 18 na kurudi kuwa ilitubidi tuondoke ghafla kwa sababu ya mechi ya Iringa ambayo hatukuwa na program nayo kwa hiyo baada ya mechi ikatubidi tuondoke usiku tena kwa sababu tuna mechi leo” amesema.
“Kwa hiyo ile kukatakata safari na nini kuna kuwa na ile uchovu, kuna kauchovu flani kalikuwepo lakini naamini kama tungekuwa katika kiwango chetu bora au tusingekuwa na uchovu tungepata matokeo mazuri tena mapema zaidi game ilikuwa tumeshaimaliza mapema” amesema.
Licha ya kauli hiyo ya Mkwasa kueleza kuwa ni uchovu, hofu ya mashabiki inatajwa kuwa inatokana na kiwango cha timu yao katika mechi 5 zilizopita ni mechi moja tu ndio imepata ushindi wa zaidi ya goli moja (3-2 vs JKT Tanzania) lakini mingine imekuwa ikipata ushindi wa goli 1-0 au sare ya 0-0, katika mechi hizo Yanga imefunga jumla ya magoli 6 na kufungwa 2
Tags
Michezo