YANGA: TUTAPINDUA MEZA KISHUJAA, MASHABIKI WATUPE SAPOTI


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa una imani ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids utakaochezwa Novemba 3 nchini Misri.

Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba kwa kufungwa mabao 2-1 jambo lililoongeza mzigo kwa Yanga ambao wanatakiwa kuifunga Pyramids mabao 2-0 ili kusonga mbele.

Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa kikosi kina morali kubwa na makosa waliyoyafanya yanafanyiwa kazi kwa ukaribu.

"Kupoteza mchezo wa kwanza haikuwa hesabu zetu kwa kuwa makosa tumeshayatambua tunayafanyia kazi na tutapambana kupata ushindi.

"Wao wametufunga nyumbani basi nasi tuna nafasi ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa marudio mashabiki watupe sapoti," amesema.

Yanga imewafuata wapinzani wao tayari kwa ajili ya mchezo huo wa marudio utakaopigwa nchini Misri.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post