STRAIKA BORA CAF MLANGONI YANGA


Mabosi wa Yanga akili zao ni kufanya Usajili matata katika Dirisha dogo la Usajili ambapo tayari jina la kiungo wa AS Kigali ya Rwanda, Haruna Niyonzima liko mezani lakini sasa kuna jina moja la straika aliyeingia Katika kikosi cha wachezaji 11 bora wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Yanga wanataka kufanya Marekebisho mazito kwenye safu yao ya Ushambuliaji, baada Ya kuona haina makali ambapo baadhi ya Mastraika wake Hawajaonyesha uwezo Mkubwa.

Mastraika hao ni Sambamba na Maybin Kalengo, Issa Bigirimana na Sadney Urikhob Ambao wameshindwa kuonyesha kile Ambacho wengi walikuwa wanakitarajia.

Sasa tayari mabosi wa Yanga wana jina la Straika Etekiama Agiti Tady ‘Daddy Birori’ raia wa Rwanda ambaye Alichaguliwa katika kikosi bora cha Afrika katika mashindano ambayo yako Chini ya Caf msimu wa 2017/18.

Straika huyo kwa sasa yuko Sagrada Esperança ya Angola ambayo Amejiunga nayo msimu huu akitokea AS Vita ya DR Congo aliyoitumikia kwa Msimu uliopita.

Habari ambazo Championi Jumatatu, limezipata na kuthibitishwa na Wakala wa straika huyo, Patrick Gakumba ni Kuwa straika huyo kwa sasa anahitajika Yanga Lakini pia Simba wamekuwa wakimuulizia.

“Huyu straika ni hatari kama ilivyo kwa Kagere (Meddie) ambaye nilimleta hapo Simba. Tayari klabu hizo mbili zinamtaka Etekiama Ambaye aliwahi kuchaguliwa na Caf katika Kikosi bora cha wachezaji 11.

“Si unamuona Kagere alivyo basi huyu ni Zaidi yake na ana uwezo wa hali ya juu wa Kufunga na tarajia kwamba unaweza kumuona Katika dirisha dogo la usajili kwa sababu Timu zote zinamuwania hadi sasa,” alisema Gakumba.

Licha ya Etekiama kuwa na uraia wa Rwanda Lakini alizaliwa nchini Congo miaka 32 iliyopita.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post