KIBARUA CHA KOCHA SIMBA CHAINGIA HATARINI


Taarifa zilizoenea zinaeleza kuwa baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems kuondoka kuelekea kwao Ubelgiji, kuna uwezekano klabu hiyo ikaachana naye.

Aussems aliondoka nchini jana kuelekea kwao ikielezwa sababu ni matatizo ya kifamilia lakini taarifa za ndani zinasema anaweza akafutwa kazi.

Inatajwa kuwa kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika mapema dhidi ya UD Songo katika hatua ya awali ndicho kinachomhukumu Aussems ndani ya Simba.

Mbali na hilo, mwenendo wa kikosi hicho licha ya kuwa na matokeo mazuri katika ligi, namna kikosi kinavyocheza hakiwafurahishi wadau wengi wa Simba pamoja na mashabiki jambo ambalo linaelezwa linaweza sababisha kibarua chake kuota mbawa.

Leo hii kikosi hicho chini ya Msaidizi wake Denis Kitambi kitakuwa na mchezo wa kirafiki majira ya saa mbili za usiku dhidi ya JKT Tanzania, mechi ikichezwa Azam Complex.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post