Ebitoke aliwinda penzi la Diamond baada ya kuachana na Mlela


Msanii wa Vichekesho Ebitoke ameamua kuvunja ukimya na kuonyesha hisia zake za mapenzi kwa Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Ebitoke ambaye siku za hivi karibuni ameachana na aliyekuwa mpenzi wake, Yusuph Mlela ameamua kuweka hisia zake wazi baada ya kwenda kwenye ukurasa ya Instagram ya Diamond Platnumz na kumuandikia ujumbe kuwa anampenda.

"Nakupenda, nikikupata nitafurahi. Siwezi kuficha hisia zangu kwa mtu ninayempenda," alieleza Ebitoke,

Hata hivyo mashabiki wa Diamond walionyesha kukerwa na Kitendo hicho cha Ebitoke na kumsihi aachane na msanii wao.

Haijulikani iwapo jitihada za Ebitoke zitafua dafu kutokana tayari na Diamond Platnumz yupo kwenye mahusiano rasmi na Tanasha Dona kutoka nchini Kenya ambapo wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post