YESU FEKI ALIYETEMBELEA KENYA AFARIKI DUNIA


Michael Job raia wa Marekani ambaye ni mhubiri na muigizaji anayeidaiwa kuwa Yesu Feki, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini.

Michael Job akiwa anaongea nchini Kenya.


Hospitali ya Heyn imethibitisha kifo hicho na wamesema alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na amefariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo.

Yesu feki alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya wiki iliyopita na alikuwa mgeni katika siku ya tamasha la dini ya wakristo nchini humo na kudanganya watu kuwa yeye ni Yesu amerudi kama alivyoahidi.

Wiki iliyopita Serikali ya nchini Kenya ilimuondoa Michael Job na kuwakamata wachungaji hao wawili  kwa kosa la kumualika Yesu huyo wa uongo.

Picha na Video zilimuonyesha Michael Job akiwa amevalia mavazi kama ya Yesu wa ukweli zilienea kwa wingi katika mitandao ya kijamii hasa barani Africa.
 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post