NIYONZIMA ARUDI KWAO RWANDA NA KUJIUNGA NA TIMU HII....


Baada ya kuvitumikia vilabu vya Simba na Yanga kwa miaka kadhaa, hatimaye Haruna Niyonzima leo  amerejea nyumbani rasmi nchini Rwanda kwa kukamilisha usajili wa kuwatumikia Mabingwa wa Rwanda Cup, Klabu ya AS Kigali inayoshiriki ligi ya nchi hiyo.

AS Kigali pia inatarajia kushiriki katika michuano ya shirikisho Barani Afrika, Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji 8 wapya wa AS Kigali, wakiwemo wanyarwanda wanne – Haruna Niyonzima, Ndayishimiye Eric Bakame, Rusheshangoga Michel, & Ishimwe Christian.

Wengine wanne ni wachezaji wawili kutoka Gabon na wawili kutoka Cameroon.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post