Tetesi za soka Ulaya Jumatano 01.05.2019: Pogba, De Ligt, Silva, Chilwell, Sessegnon

Paul Pogba

Real Madrid haijajiandaa kumlipa mshahara wa £290,000 kwa wiki kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba na kwamba mchezaji huyo atalazimika kuchukua kiwango cha chini iwapo anataka kujiunga na miamba hiyo ya Uhispania. (ESPN)
Beki wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, anataka kujiunga na mwenzake Frenkie de Jong katika klabu ya at Barcelona msimu ujao lakini Ajenti Mino Raiola angependelea mchezaji huyo kujiunga na Man United , Juventus ama Bayern Munich. (Mundo Deportivo)
Kiungo wa kati wa Manchester City Bernardo Silva
Kiungo wa kati wa Manchester City Bernardo Silva, 24, anasema kwamba hajafikiria kuondoka katika ligi ya Premia , licha ya ripoti zinazomuhusisha na mabingwa wa Uhispania Barcelona. (Manchester Evening News)
Arsenal wameambiwa watalazimika kulipa kitita cha £17.2m ili kumsaini mshambuliaji wa PSG ,21, Christopher Nkunku . (Evening Standard)
Manchester City haitamwania beki wa kushoto wa Leicester City na Uingereza Ben Chilwell, 22, kwa sababu wanawamiliki wachezaji mbadala Benjamin Mendy na Oleksandr Zinchenko. (Manchester Evening News)
Tottenham wanaongoza harakati za kumsajili kijana wa Fulham Ryan Sessegnon
Tottenham wanaongoza harakati za kumsajili kijana wa Fulham Ryan Sessegnon, ambaye pia anazivutia klabu za Paris St-Germain, Juventus na Borussia Dortmund baada ya klabu hiyo kushushwa daraja kutoka ligi ya Premia. (Evening Standard)
Inter Milan inajianda kumnunua beki wa Man United Matteo Darmian, 29, kurudi Itali , huku klabu hiyo ya Uingereza ikiwa tayari kumuachilia kwa chini ya dau la £9m. (Gazzetta dello Sport, via the Sun)
Kiungo wa kati wa Chelsea aliyeko katika mkopo katika klabu ya AC Milan Tiemoue Bakayoko, 24, anataka kurudi katika uwanja wa Stamford Bridge - na kutoongeza kandarasi yake na mabingwa hao wa Setrie A baada ya kurushiwa maneno ya kibaguzi nchini Itali. (La Republicca, via the Sun)
Kiungo wa kati wa Chelsea aliyeko katika mkopo katika klabu ya AC Tiemoue Bakayoko,
Mkufunzi wa klabu ya Rangers Steven Gerrard anamtaka mshambuliaji wa Watford Andre Gray, 27, kuongoza kikosi chake kuwania taji la ligi ya uskochi msimu ujao na klabu hiyo ya ibrox itajaribu kumnunua kwa mkopo. (The Herald)
Mkufunzi wa West Ham Mauricio Pellegrini amemtaja beki wa kati wa klabu ya Alaves Guillermo Maripan, 24, na beki wa kushoto wa Olympiakos Leonardo Koutris, 23, kama mchezaji wanayemlenga kuimarisha safu ya ulinzi (Football.London)
Beki wa Crystal Palace Mamadou Sakho, 29,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Beki wa Crystal Palace Mamadou Sakho, 29, amesema kuwa huenda akaondoka katika klabu hiyo baada ya kusema kwamba anataka kucheza soka ya vilabu bingwa Ulaya(Telefoot, via Croydon Guardian)
Newcastle inataka kumsaini mshambuliaji wa Venezuela mwenye umri wa miaka 19 Jan Carlos Hurtado - ambaye amepokea sifa kutoka kwa mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Faustino Asprilla - kutoka kwa timu ya Argentina Gimnasia. (Newcastle Chronicle)

TETESI ZA SOKA JUMANNE

David De Gea
Paris St-Germain inafikiria kumnunua kipa wa Manchester United davdi De Gea kwa dau la £90m huku kipa huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 akitarajiwa kulipwa £450,000 kwa wiki na mabingwa hao wa Ufaransa. (Star)
Manchester United inajiandaa kumnunua kipa wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26 Jan OBlack. (ESPN)
Mchezaji wa zamani wa Man United na Uingereza Rio Ferdinand amekutana na naibu afisa mkuu mtendaji Ed Woodward ili kuzungumzia kuhusu kuwa mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo (Mail)

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post