KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa wachezaji wake walishindwa kufuata maagizo kipindi cha kwanza hali iliyowafanya walazimishe sare ndani ya dakika 45 dhidi ya Tanzania Prisons, uwanja wa Uhuru licha ya kushinda kwa mabao 2-1.
Prisons walisawazisha bao la Pappy Tshishimbi lililofungwa dakika ya 23 baada ya dakika 10 za kipindi cha kwanza kupitia kwa Ismail Kada.
Zahera amesema kuwa mbinu yake ilivurugwa na wachezaji wake kipindi cha kwanza hali iliyofanya wakawa sare ndani ya dakika 45.
"Dakika 45 za mwanzo hatukucheza vizuri, wachezaji wangu walivuruga maelekezo yangu ndio maana tulifungwa, ila baada ya kuwaweka sawa kipindi cha pili walitakata hivyo ndivyo ilivyotakiwa tufanye.
"Wapinzani wetu walikuwa wazuri na wanapambana ila tulitakiwa nasi tuwabane ili kushinda, goli letu la pili limetoka pembeni hivyo inamaanisha wachezaji walifunguka, nawapa pongezi kwa ushindi," amesema Zahera.