![Barcelona wanamtaka mchezaji wa Manchester United safu ya mashambulizi wa Marcus Rashford](https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/65F4/production/_106600162_fb95900c-7b30-4c3c-a201-429b00997125.jpg)
Barcelona wamejiandaa kumuhamisha kwa £100m mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21. (Mail)
Inter Milan will wanajiandaa kwa uhamisho wa mchezaji wa Manchester United Alexis Sanchez ikiwa raia huyo wa Chile mwenye umri wa miaka 30 ataachanana madai ya mshahara. (Independent)
Chelsea wanaangalia uwezekano wa kunchukua mchezaji mahiri wa Barcelona Mbrazili Philippe Coutinho, ikiwa watampoteza Eden Hazard this summer. Hazard, mwenye umri wa miaka 28, anahusishwa na taarifa za uhamisho wa kuelekea Real Madrid na the Blues wanamuona Coutinho mwenye umri wa miaka 26- kama mtu anayefaa kuchukua nafasi yake kama vikwazo vya uhamisho vitachelewa. (El Confidencial)
![Chelsea wanaangalia uwezekano wa kunchukua mchezaji mahiri wa Barcelona Mbrazili Philippe Coutinho](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/8D04/production/_106600163_b0a69b10-5b28-4fd3-90a0-0ab3e30f45b6.jpg)
Mshmbuliaji wa kati wa Everton na Brazil Richarlison, mwenye umri wa miaka 21,ni mchezji wa hivi karibuni kuangaliwa na Manchester United kama sehemu kubwa ya kukarabati kikosi chao kilichofeli msimu ujao. (Telegraph)
![Inter Milan will wanajiandaa kwa uhamisho wa mchezaji wa Manchester United Alexis Sanchez](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/DB24/production/_106600165_41cdbb98-658d-44b8-95ad-b768619b0247.jpg)
Naibu wenyekiti mtendaji wa klabu ya Manchester United Ed Woodward alifanya mazungumzo juu ya mzozo na meneja Ole Gunnar Solskjaer na naibu wake Mike Phelan katika uwanja wa klabu hiyo wa mazoezi kufuatia kushindwa mara ya saba katika mechi nane za Manchester. (Mail)
Atletico Madrid wanapanga kumuhamisha mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United Muhispania Juan Mata, mwenye umri wa miaka 30. (Sport)
![Atletico Madrid wanamtaka Muhispania Juan Mata anayechezea Manchester United](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/10234/production/_106600166_92d3a837-b9fe-4877-8d34-bb26c484ec3d.jpg)
Arsenal wanapanga kuongeza uhasama na mahasimu wao katika Primia Ligi Everton kwa kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Barcelona Mreno Andre Gomes, mwenye umri wa miaka 25. (ESPN)
Arsenal wana nia ya kusaini mkataba na mlinzi wa Manchester United na Ivory Coast Eric Bailly, mwenye umri wa miaka 25. (mail)Leicester kw aupande mwingine wanachunguza kwa makini uwezekano wa kusaini mkataba na mshambuliaji wa Atalanta na Italia Andrea Petagna, 23. (Guardian)
West Ham wanapima uwezekano wa kumuhamisha Mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid Muhispania Dani Ceballos, mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)
![West Ham wanapima uwezekano wa kumuhamisha Mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid Muhispania Dani Ceballo (kulia)](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/12944/production/_106600167_a4b1f4d1-70b2-419a-971b-e00a8db3ef25.jpg)
Mshambuliaji wa Southampton Shane Long, mwenye umri wa miaka 32, anaamini kuwa anacheza kwa ajili ya siku zijazo katika klabu hiyo.(Daily Echo)
Wolves wametoa maombi juu ya mlinzi wa Besiktas na roatia Domagoj Vida, mwenye umri wa miaka 29. (Sporx - via Sport Witness)
![Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye anachezea Manchester United Romelu Lukaku anasema itakuwa ni ''ndoto'' kwake kucheza nchini Italia](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/15054/production/_106600168_f61c98d4-47ba-4dc8-ab76-8525023a9b1e.jpg)
West Ham wanapima uwezekano wa kumuhamisha Mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid Muhispania Dani Ceballos, mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye anachezea Manchester United Romelu Lukaku anasema itakuwa ni ''ndoto'' kwake kucheza nchini Italia . (Sky Italia - via Metro)
Arsenal watasaini mkataba na Mshambuliaji wa kati Mbrazili Gabriel Martinelli mwenye umri wa miaka 17 kutoka klabu ya Ituano msimu ujao. (Goal)