NJIA 16 ZA KUMFANYA MPENZI WAKO ASHIKAMANE NAWE


Epuka hasira;

Usishughulikie changamoto kwa hasira, jazba na mhemko. Kwa asili binadam hapendi kushambuliwa hata kama ana makosa. Usimkabili mpenzi wako ukiwa na hasira. Kama unataka matokeo mazuri, basi subiri pale mtakapokuwa mmetulia hapo utaweza kumkabili na kuzungumza naye kwa utulivu. Moja kwa moja utamuona akilifikiria jambo hilo kwa utulivu huku akijilaumu. Hii ni njia bora kabisa ya kushughulikia changamoto za mahusiano. Kadhalika iwapo mpenzi wakoamefanya kosa usisahau kuwa anayo mazuri pia. Miongoni mwa sababu kubwa za wapenzi kuachana ni pale wanapojikita kwenye mabaya na kusahau mazuri ya upande wa pili.

Epuka kumAibisha mbele ya watu;

Hakuna kitu kinachomkasirisha mtu kama mpenzi anayemkera na kumuaibisha mbele ya watu, mbele ya marafiki na jamaa zake. Jambo hilo huwa na taswira hasi kwenye saikolojia ya mtu hata kama ulikusudia kufanya utani tu. Huwezi kujua reaction yake kwa ulichokifanya. Hivyo, epuka sana jambo hilo ili mahusiano yenu yasonge mbele kwa amani.

Epuka kupiga makelele:

Unapotaka kuwasilisha hoja yako tumia sauti, usitumie kelele. Hakika sauti mbaya zaidi ni sauti ya punda, basi usiifanye hoja yako kutawaliwa na sauti kama ya punda badala ya sauti maridhawa iliyojaa madaha na umaridadi wa kimahaba.

Acha kumpigia makelele mpenzi wako na kumkumbusha kasoro zake kila mara, kwa sababu hakuna mtu mkamilifu, na upendo wa kweli hujengwa kwenye kustahmiliana na kuvumilia kasoro za mwenzako. Usijaribu kuyalinganisha mazuri ya watu wengine na yale ya mpenzi wako. Hao wengine unayajua mapungufu yao? Je, huyo unayemlinganisha na mpenzi wako umeziona kasoro zake na mpenziwe? Usimfanye mpenzi wako ajihisi duni kwa kasoro zake, bali muoneshe kwamba licha ya kasoro zake bado ni Majnun wako.

Vitendo vya kimahaba vitawale mahusiano yako:

Mahusiano mengi hufa kwa sababu zinakosa vitendo vya kimahabba kutoka kwa wapenzi husika. Hakika vitendo hivyo humuonesha mpenzi wako kuwa unafurahia kuwa naye. Vitendo vya kimahabba ni zaidi ya tendo la ndoa. Vitendo vya kimahabba huakisi ulimwengu wako wa ndani. Pumzi zako huwa romantic, maneno na kauli zako huwa romantic, mapishi yako huwa romantic, mavazi yako huwa romantic, chumba chako huwa romantic, maji ya kukoga huwa romantic…. Hakika kila kitu chako huonesha umaridadi wako wa kimapenzi.

Usiwe kama bosi wake:

Usijaribu kumwambia mwenza wako anachotakiwa kufanya kazini kwake. Anapokuwa amekosea jambo fulani kazini, usijaribu kumkosoa na kumnanga, bali msikilize na umpe moyo wa kukabiliana na changamoto hiyo. Mwambie kuwa unaamini anaweza kuitatua.

Mfanye kuwa kipaumbele chako:

Unapoingia kwenye mahusiano, basi mtu ambaye anapaswa kuwa namba moja katika maisha yako ni mwenza wako. Sio kazi yako wala familia yako. Kwa kufanya hivo utamfanya mpenzi wako ajihisi ni wakipekee zaidi na azidishe upendo wake kwako na ashikamane nawe zaidi na hivyo kuyafanya mahusiano yenu yadumu zaidi na zaidi.

Fikiria hayo.

  Install Application ya UFUNDI KITANDANI Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post