Yanga ilivyojiandalia faini ya laki 5 au milioni 1



Katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara jana, dhidi ya wenyeji wao Coastal Union wachezaji wa Yanga waliingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi katika mchezo wake dhidi ya Coastal Union uliopigwa katika dimba la Mkwakwani, Tanga .
Licha ya jambo hili kukemewa na timu kupigwa fainali hivi karibuni lakini inaonekana haisadii na timu inakuwa tayari kufanya hivyo ikiamini italipa fainali jambo ambalo linabaki kwa TFF.
Sio Yanga tu timu nyingibza ligi kuu na ligi daraja la kwanza zimekuwa zikitumia utaratibu huu ambao mara nyingi unahusishwa na imani za kishirikina!.
Hivi karibuni bodi ya ligi ilizipiga faini klabu kadhaa ikiwemo Singida United kufuatia kushindwa kuingia kwenye vyumba vya kubadiishia nguo kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam walipocheza na Simba huku wakitumia chumba cha wanahabari kubadilishia nguo.
Katika mchezo wake wa jana na Coastal Union, Yanga ililazimisha sare ya bao 1-1. Bao la Coastal Union lilifungwa na Haji Ugando dakika ya 29 huku lile la Yanga likifungwa na Matheo Anthony dakika ya 76.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post