Picha ya Ebitoke yaibua Hisia Kali Kwa Mashabiki


Mashabiki wameiponda vikali picha ya Ebitoke ambayo imeonyesha mwili wake kwa kiasi kikubwa kitu ambacho hakizoeleka kutoka kwake.

Mchekeshaji huyo amechapisha picha hiyo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram na kuwauliza mashabiki wake wanainaje.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameikosoa vikali huku wachache wakipongeza. Chini ni baadhi ya mashabiki wake waliotoa maoni yao.


Fanuel Kelly - Toka lini ukawa mweupe hivyo,unajiharibu bora ubaki na rangi yako.

Collin Aggy - Bukoba walikufundisha kuvaa ivo?naona ushaiga tabia za mjini.

Shawn Kings20 - Hayo mambo sio fani yako Ebitoke, Kimwili chenyewe kimejaa makovu kwa jembe.

Ebitoke alijizolea umaarufu mkubwa ndani ya kundi la Timamu akiwa na wachekeshaji wengine kama Mkaliwenu, Bwana Mjeshi, Mamaa Ashura, kwa sasa Ebitoke ameondoka kwenye kundi hilo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post