Snoop Doddgy aingia kwenye anga za Snura, apost wimbo wake


Msanii na na mwandaaji nguli wa muziki nchini marekani Snoop Doggy amedondosha shavu kwa  msanii wa kike nchini Tanzania, Snura Mushi kwa kuipost ngoma yake ya Zungusha kwenye ukurasa wake wa instagram.

Snoop ameonyesha kuipenda jinsi inavyochezwa baada ya kipande cha video kusambaa na hatimaye kumfikia ambapo alionyesha kupendezwa na kuiweka kwenye ukurasa wake.

Snura mushi amefurahishwa na kitendo cha msanii huyo mkubwa kuposti nyimbo yake hiyo kwenye ukurasa wake na kuahidi kuwa ataendelea kufanya kazi nzuri.

Katika pita pita ya huku na kule baada ya snoop kuweka kipande hiko cha wimbo na kuonekana hajui asili ya hiyo nyimbo mtangazaji kutoka clouds Mami baby alimvutia kwa kukoment chini na kumueleza msanii huyo nguli kutoka marekani kuwa ngoma hiyo ni kutoka Bongo

Kama ulikuwa hujui nikujuze snura mushi ni msanii wa bongo fleva ambae anafanya vizuri kwenye soko la muziki nchini kwa mtindo wa nyimbo zake zenye mahadhi ya uswazi na kabla ya kuingia kwenye muziki alikuwa kwenye sanaa ya filamu ambapo umaarufu zaidi aliupata kwenye tamthiliya ya Jumba la dhababu.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post