Mourinho atamkimbiza Sanchez Man United


Mshambuliaji wa kimataifa wa Chileanayeichezea Club ya Man United ya EnglandAlex Sanchez ameripotiwa kutaka kuihama club hiyo, akiwa amedumu nayo kwa miezi tisa pekee toka alipojiunga nayo akitokea Arsenal.

Wawakilishi wa Sanchez wamekuwa wakiripotiwa kufanya mazungumzo na vilabu kadhaa ili kuhakikisha staa huyo anaondokaMan United, kwani Sanchez msimu huu amekuwa na wakati mgumu ndani ya club yaMan United ukizingatia kwa sasa timu inacheza mfumo wa kujihami zaidi ambayo ndio falsafa ya kocha wao Jose Mourinho.

Hata hivyo baadhi ya stori za chini kwa chini zimekuwa zikidai kuwa mpenzi wa staa huyo Mayte Rodrigruez amekuwa ni chanzo cha kuathiri uwezo wa staa huyo uwanjani,Jose Mourinho amekuwa akimuacha njeSanchez msimu huu kwa zaidi ya nusu ya mechi zote za Man United msimu huu.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post