Kijana wa miaka 21 ambaka bibi wa miaka 85

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita amethibitisha kuwa wanamshikilia Daniel Colner mwenye umri wa miaka 21 kwa tuhuma za kumbaka bibi kizee wa miaka 85.

Image result for african old lady

Akiongea na wanahabari leo Oktoba 17, mkoani humo Kamanda Koka amesema tukio hilo limetokea Oktoba 15 katika Kata ya Kingachi wilayani Rombo, ambapo Daniel alivunja mlango wa nyumba ya bibi huyo na kumbaka.
''Bibi alifikishwa kituoni na baada ya uchunguzi wa awali ilbainika ameingiliwa kinguvu na kuachiwa manii sehemu za siri lakini uchunguzi zaidi unaendelea wakati kijana huyu anayetuhumiwa tukimshikilia kwa mahojiano'', amesema Kamanda Moita.
Kamanda ameeleza kuwa baada ya kufanya kitendo hicho cha ubakaji, taarifa za tukio hilo ziliripotiwa katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya Rombo na askari kuanza msako mara moja na kufanikiwa kumkamata Daniel.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post