Jack Wolper Kuwa Mpambaji wa Ikulu..



STAA wa Bongo Movie, Jackline Wolper, amesema moja ya ndoto zake kubwa ni pamoja na kuja kuwa mpambaji wa kimataifa ikiwemo Ikulu.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Wolper alisema watu watambue kuwa ana kipaji kikubwa cha kupamba na alianza nacho kabla ya kuwa mwigizaji  na mjasiriamali.

“Mashabiki zangu wachache wasiojua mimi ni mpambaji wa shughuli mbalimbali, nilianza zamani na watu walikuwa wakikubali kazi zangu, ninachoomba kwa Mungu ni uzima na afya kwakuwa nimepanga kutafuta kazi hadi Ikulu,” alisema Wolper.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post