ZIDANE ATAJA WACHEZAJI WAKE MAN UNITED, MOURINHO PRESHA JUU

Image result for zidane vs mourinho

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Zinedine Zidane,  ambaye hivi sasa hajapata ajira, ametaja baadhi ya wachezaji muhimu ambao anaweza kuwatumia iwapo atafanikiwa kuwa kocha wa klabu ya Manchester United ya Uingereza.

Zidane ambaye ameipa mafanikio makubwa Madrid, inayojulikana kama Los Blancos, amewataja wachezaji Kroos, Thiago Alcantara, James Rodriguez na Edinson Cavani ambao alisema wako tayari kuungana naye katika klabu ya Manchester iwapo atamrithi kocha wa sasa Jose Mourinho.

“Ni kweli, nitarejea tena kwenye kufundisha, kwani ndiyo kazi ambayo nimeifanya siku zote hadi sasa,” alisema Zidane alipohojiwa na kituo cha televisheni cha TVE.

Mourinho hivi sasa yuko chini ya shinikizo kufuatia  klabu hiyo kufanya vibaya msimu uliopita na ambapo hadi sasa imepoteza michezo miwili miongoni mwa minne iliyocheza katika ligi kuu ya Uingereza.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post