Baba Mzazi wa Davido Alituma Polisi 50 Wamtoe Davido Stejini

Staa Davido ambaye pia ni mmiliki wa record label ya Davido Music Worldwide “DMW” kupitia mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha redio cha The Breakfast Club September 4,2018 amefunguka kuhusiana na safari yake ya muziki.

Davido amefunguka pia kuhusiana na maisha ya baba yake kutofurahishwa na yeye kuacha chuo na kujiingiza kwenye masuala ya muziki na hivyo kusema kuwa baba yake aliwahi kutuma polisi 50 ili wamkamate kwenye show yake ya  kwanza ambayo aliifanya akiwa Nigeria.

“Baba yangu aliwahi kutuma polisi 50 kwenye show yangu ya kwanza ili wanikamate lakini niliruka fensi na kutoroka lakini walibahatika kumkamata aliyekuwa mpenzi wangu na promota wa show yangu, baba alinipigia simu na kusema nisipojitokeza basi atawapeleka jela”

Davido aliongeza na kusema kuwa mama yake mzazi alifariki akiwa na miaka 11 kwahiyo maisha yake yote amekua akiishi na baba yake. Davido alizaliwa Marekani lakini alipofikisha miaka miwili walirudi nyumbani Nigeria lakini baadae alirudi Atlanta Marekani  kwaajili ya masomo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post