AFC LEOPARDS YAIBUA MSALA SIMBA, TFF WAWEKA ANGALIZO



Image result for afc leopards

Na George Mganga

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawakumbusha Wanachama wake kwamba hairuhusiwi timu ya Mpira wa Miguu kutoka nje ya nchi kucheza mechi ya kirafiki au kushiriki mashindano hapa nchini bila ya kibali kutoka TFF na pia kukamilisha taratibu zilizowekwa na FIFA.

TFF imesema kuwa ni vema kwa vilabu hivyo kufanya taratibu hizo ambazo zimewekwa kwa mujibu wa shirikisho pamoja na FIFA.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano, Salum Madadi, amesema wamefikia hatua ya kuzikumbusha timu ikiwa ni baada ya Simba kuwaalika AFC Leopards ya Kenya kuja nchini kucheza bila kufuata taratibu maalum.

Madadi amesema suala hilo la Simba limewashtua wengi na kufikia maamuzi ya kuwaamua kulikumbushia tena ili kuweka mambo sawa.

"Tumeamua kulikumbushia hili kulingana na hivi karibuni kuna timu mbili kutoka nje ya Tanzania zilikuja kucheza na Simba pamoja na Biashara United bila kufuata taratibu rasmi ambazo zimewekwa kwa mujibu wa TFF na FIFA" alisema.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post